JIFUNZE KUZIFAHAMU NA KUZIKUBALI NYAKATI ZA MAISHA YAKO




.
Moja ya changamoto kubwa utakutana nayo maishani mwako ni pale ambapo watu wanaokuzunguka wanakutarajia uishi maisha ambayo fika unaona sio saizi yako.Ni muhimu kukumbuka kuwa kwa kila majira ya Maisha YAKO kuna mambo unatakiwa kuyafanya.Leo Ngoja nikushirikkishe nyakati mbili:
.
1)WAKATI WA KUJENGA MSINGI/KUPANDA MBEGU
.
Huu ni wakati wa kujinyima mambo mengi sana na mara nyingine watu wanaweza wasikuelewe.Mara nyingi unachopata hapa sio kwa ajili ya matumizi ya kila siku bali kiasi kikubwa ni kama MBEGU ambayo ukiiweka itakubidi usubirie Muda mrefu sana kabla haujaona matokeo yake.
.
Katika kipindi hiki pia unaweza kuona NGUVU na MATOKEO hayaendani kwa sababu bado ni wakati wa KUMWAGILIA MBEGU yako.Ukiingia kwenye jaribu la kutaka kuonyesha UNAVUNA TAYARI,hapo utapoteza mwelekeo haraka.
.
2)WAKATI WA KUINGIZA BIDHAA/ZAO SOKONI.
.
Kumbuka kuna watu walishatangulia kabla yako,kuna watu ambao Hawakuamini sio kwa sababu HAUNA UWEZO ila kwa sababu HAWAKUJUI,hawajawahi kukusikia.
.
Huu ni wakati ambao UTASHANGAA na UTAUMIA kwa sababu kuna watu wenye uwezo mdogo kuliko wewe wanapewa nafasi na wewe haupewi.Huu sio wakati wa kulazimisha NAFASI ni wakati wa KUONGEZA MATOKEO.Kumbuka kazi yako hapa ni kujenga “Credibility” ili wakuamini.
.
Je umeshawahi kupitia nyakati yoyote kati ya hizi?
.
See You At The Top



Want the inside scoop

JOIN THE COMMUNITY


Copyrigh © 2018  JOEL NANAUKA   All Rights Reserved