Mbinu Ya Kutumia Ili Kutimiza Malengo Yako
Unataka kujihakikishia kutimiza Malengo yako uliyojiwekea-John Maxwell anasema-“Mafanikio unayoyatafuta yamejificha katika mafanikio unayopata kila siku”.Leo unataka kufanikiwa katika lipi?
.
Watu wengi sana huwa wanaamini katika kupata mafanikio Makubwa kwa siku moja au Muda mfupi-Kwa sababu hiyo huwa wanadharau kile wanachoweza kukifanya kwa siku fulani.
.
Make everyday count:Leo ina mchango mkubwa sana wa mafanikio makubwa unayoyatafuta.Kabla siku haijaendelea sana jiulize swali:Hivi leo kuna Kitu gani ambacho nitakifanya Chenye mahusiano na MALENGO MAKUBWA ya MAISHA yangu?
.
Ukiona leo umeamka,unakula,unafanya mambo tu ya kawaida kisha usiku ukifika unalala basi ujue siku ya leo UMEIPOTEZA.Ifanye leo ichangie mafanikio YAKO kwa kufanya kitu hata kama ni kidogo.Usikubali kuishi kwa MAZOEA.
.
Je,Leo utafanya Nini kinachochangia katika mafanikio yako?Niambie hapo chini
.
See You  at The TopWant the inside scoop

JOIN THE COMMUNITY


Copyrigh © 2018  JOEL NANAUKA   All Rights Reserved