Njia Mbili za Kuongeza Kipato Chako
Umeshawahi kujiuliza,nitawezaje kuongeza pesa ambayo naipata katika maisha yangu?Watu wengi sana huwa wanatamani kuongeza kipato cha ila huwa wanatumia njia ambazo sio sahihi kuongeza kipato.Leo ningependa ujifunze njia rahisi ambazo unaweza kuzitumia mara moja kuanza kuongeza kipato chako na kujihakikishia ongezeko la kipato chako kwa haraka zaidi.

Jambo la kwanza la kujiuliza unapotaka kuongeza kipato chako ni kuwa,uko tayari kutatua matatizo ya watu?Sehemu mojawapo kubwa ambayo pesa imejificha ni kwenye matatizo ambayo yanawakabili watu mbalimbali,na leo utajifunza mbinu za kuchukua pesa zilizojificha huko.

Tafsiri kubwa ninayopenda kuitumia kuhusu pesa ni ile inayosema-“Pesa ni zawadi unayopata baada ya kutatua tatizo la mtu fulani”.Kwani huu ni ukweli ambao hauwezi kupingika kabisa,ukitaka kujua tafasiri hii imebeba uzito mkubwa kwenye maisha yako jiulize swali-Je,tangu leo umeamka umetumia pesa yako kufanya mambo gani?Jaribu kuorodhesha na kwa kila matumizi uliyofanya utagundua kuwa kuna mtu ulimlipa ambaye amekutatulia tatizo lako ambalo wewe hauna uwezo wa kutatua ama hauna muda wa kutosha kulitatua,hivyo umeruhusu mtu afanye kwa niaba yako.

Hii maana yake ni kuwa njia kubwa ya kwanza ya kupata pesa ni kutatua tatizo/matatizo ambayo yanawakabili watu fulani kwenye eneo lako.Kadiri unavyotatua matatizo mengi zaidi ndivyo utakavyokuwa unazidi kuvutia pesa nyingi kwa upande wako.Kadiri unavyotatua matatizo makubwa ndivyo pia utakavyokuwa unavutia pesa kubwakubwa kwenye maisha yako.Hii ina maana ukijigundua kuwa unaingiza pesa kiasi kidogo uwezekano mkubwa ni kuwa haujatatua matatizo ya kutosha.

Kila unapopita kuna matatizo yanayowakabili watu na kazi yako ni kuchagua aina ya tatizo ambalo unaona liko ndani ya uwezo wako kulitatua na kuanza kulifanyia kazi mara moja.Kwa hiyo kabla haujaendelea mbele zaidi kusoma,jaribu kujiuliza swali hili:”Hivi kwenye mazingira yangu kuna tatizo gani ambalo naweza kulitatua?”.Hii haijalishi kama uko eneo la shule,ama uko eneo la kazi au uko eneo la biashara.Jaribu kuorodhesha kila tatizo ambalo watu wanakabiliana nalo katika eneo lako na jiulize-Je,naweza kulifanyia kazi lipi kati ya hili?Wakati mwingine unaweza kuamua kuuliza watuw anaokuzunguka kuhusiana na changamoto zinazowakabili na watakuambia,kumbuka kuwa wazo bora kabisa la biashara ni lile linalolenga kutatua matatizo yanayowakabili watu wa eneo husika.

Je,umeshapata tatizo ambalo unaweza kulitatua?Wengi huwa wanasema wanakwamisha na mtaji,ila katika kuchagua tatizo hakikisha unaanza na lile ambalo unaweza kuanza nalo kwa kile ulichonacho.Hakikisha wiki hii haiishi kabla haujaanza kulifanyaia kazi wazo hili ambalo umelipata,ukichelewa sana utakuta kuna mtu mwingine ameshalifanyia kazi mara moja haraka.

Njia ya pili ya kuongeza kiwango cha pesa ambazo unazipata ni kuhakikisha kuwa unaongeza thamani yako katika kile unachokifanya.Unachotakiwa kujua ni kuwa watu hukulipa pesa kulingana ana thamani ambayo unaitoa,hii inamaanisha unaweza kufanya kazi kwa bidii lakini kama hauongezi thamani yako basi malipo yako yanaweza yasiongezeke kabisa.Kuna tofauti kubwa ya kufanya kazi kwa nguvu na bidii (Working Hard) na kufanya kazi wa werevu na maarifa (Working Smart).Hii ya pili hutoa matokeo makubwa sana nay a haraka kwa mtu anayetumia wakati ile ya kwanza hutoa jasho jingi ila matokeo huwa ni machache sana.

Hebu jaribu kujichunguza kwenye maisha yako,wewe ni mtu ambaye unafanya kazi sana lakini matokeo ya kifedha ni madogo?Je,ni mtu ambaye si mvivu,unaamka mapema asubuhi na unachelewa kulala ila ukiangalia muda uliofanya kazi na mafanikio ya kifedha uliyoyapata hayalingani kabisa?Kama wewe ni mmojawapo inamaanisha inawezekana uko kwenye kundi hili.Hata hivyo kuna njia kadhaa ambazo unaweza kuzitumia kuongeza thamani yako.

Moja ni kuongeza ujuzi wa kile unachokifanya.Hivi umeshawahi kujiuliza kwa nini wachezaji wanawecheza timu moja ndani ya dakika tisini lakini kuna mwingine analipwa zaidi ya mwingine?Jibu ni kuwa anayelipwa zaidi ingawa anatumia muda uleule ila ana ujuzi ambao wengine bado hawana kwenye maisha yao.Moja ya changamoto ya watu wengi katika mambo wanayofanya ni kuwa hawaongezi ujuzi kabisa matokeo yake hawaongezi kipato kabisa.

Hebu jaribu kujiuliza-Katika unachofanya leo,ni lini mara ya mwisho uliongeza ujuzi?Ulijifunza kitu kitu kipya mtandaoni?ulihudhuria kozi?ulipata mafunzo fulani?Kama ujuzi wako ni uleule kama ulivyokuwa mwaka jana uwe na uhakika pia malipo yako ya kipesa yatabakia vilevile.Kumbuka kuwa tumeshahama kwenye ulimwengu wa watu kutumia UZOEFU wao tuko kwenye ulimwengu wa watu kutumia UJUZI wao.Bila kujali uanfanya kazi gani au biashara gani na una muda mrefu kiasi gani.Leo jiulize,je kuna ujuzi gani ambao natakiwa kuuongeza katika maisha yangu ambao nikwia nao utaniongezeka kasi ya matokeo?Jaribu kutafakari kabla haujaendelea.

Ukishaujua ujuzi huo,jipangie mkakati wa namna ya kuuongeza haraka.Inawezakena ikakulazimu kusoma kozi rasmi,kwenda kwa mtu kujifunza ama kutumia mtandao.Kwa vyovyote vile,hakikisha unajiwekea mkakati wa kuongeza ujuzi kwa haraka.Ningependa kusikia toka kwako pia aina ya ujuzi ambao umekusudia kuuongeza.

Mbili,ili kuongeza thamani yako upate kipato zaidi ni kuhakikisha kuwa unajenga sifa ya kuaminika kwa kila jambo.Kati ya vitu ambavyo vinakata mifereji ya pesa kwenye maisha ya watu wengi ni hali ya kushindwa kuaminika.Watu wakishasema wewe ni mtu usiyeaminika ina maanisha ni moja kwa moja hawatakuwa tayari kukupa pesa ama fursa zaidi.

Kumbuka kuwa kuna watu wanaweza kukuamini na kukuzima pesa hata bila kuandikishana kwa sababu wanajua utawarudishia,ila ukivunja uaminifu ni ngumu kuurudisha.Jitahidi kila wakati kujenga sifa ya kuaminika-Kama unafanya biashara wafanye wateja wakuamini kwa kutimiza ahadi unazowapa,kwa kuwapelekea bidhaa kama mlivyokubalina na kwa ubora uliowaambia.Kama wewe umeajiriwa,jitahidi kuwa na sifa ya kuaminika kwa kufanya kazi yako kwa wakati,kutotumia uongo n.k

Leo,jiulize-Nawezaje kujenga uaminifu katika kile ninachofanya ili nivutie pesa zaidi?


 


 

Joel Arthur Nanauka

YouTube:Joel Nanauka

Facebook:Joel Nanauka Page

Instagram:joel_Nanauka

jnanauka@gmail.com

0655 720 197


 Want the inside scoop

JOIN THE COMMUNITY


Copyrigh © 2018  JOEL NANAUKA   All Rights Reserved